Ticker

6/recent/ticker-posts

Wizikid Anakula Sahani Moja na Meneja Wake...Watarajia Kupata Mtoto wa Pili


Habari njema kwa mashabiki wa Star Boy Big Wiz @wizkidayo ni kwamba nyota huyo anatarajia kupata mtoto wa pili na baby mama wake Jada Pollock maarufu Jada P ambaye pia ni meneja wake. Jada P amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram.


Itakumbukwa, Jada P alikutana na Wizkid mwaka 2012, ambapo wakati huo Jada alikuwa bado anamsimamia mwimbaji maarufu wa Marekani, Chris Bown. Baadae akawa meneja wa Wizkid lakini uhusiano wao ukawa zaidi ya kazi.


Mwaka 2017 walipata mtoto pamoja ambaye ni mtoto wao wa kwanza aitwae "Zion" mwenye umri wa miaka 4 sasa.


Hata hivyo, huyu ataenda kuwa mtoto wa nne kwa WizKid baada ya kuwa na watoto wengine wawili aliowapata toka kwenye mahusiano yake yaliyopita akiwa na Shola Ogudugu na Binta Diamond.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments