Geita Gold Waapa Kuifunga Simba, Nahodha Wao Asema Hawata Wadharau

 


KLABU ya Geita Gold yenye makazi yake mjini Geita inaenda kushusha karata yake ya kwanza katika mchezo ya ligi kuu dhidi ya klabu ya simba.


Mchezo huo unaonekana kwenda kuwa mgumu kutokana na timu zote mbili kuwa na kiwango kizuri huku mfungaji bora wa msimu wa 2021/2022 George Mpole anatokea katika klabu hiyo ya Geita.


Kocha wa Geita Gold amesema kuelekea mchezo huo wamejiandaa vizuri na wapo tayari kufanya makubwa katika mechi hiyo.


Amesema klabu ya Simba ipo vizuri na ina wachezaji wazuri lakini simba wanafungika tu na wanataka kupata matokeo ya ushindi dhidi ya simba.


Naye nahodha wa timu Hiyo Kelvin Nashon amesema wachezaji wote wapo vizuri na wamejiandaa kwenda kupata matokeo ya ushindi japo Simba ina wachezaji wenye viwango vya juu lakini watawaheshimu na hawatawadharau kutokana na matokeo walioyapata kwenye ngao ya jamii.

Klabu hizi mbili zimekutana mara mbili huku klabu ya Simba ikiwa imeshinda mchezo mmoja na kutoa sare mchezo mmoja.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad