Ticker

6/recent/ticker-posts

Kimenuka..Rais Uhuru Kenyatta Amshukia RUTO "Sina Haja ya Kukuua, Ningetaka Uwezo Nilikuwa Nao"


Rais Uhuru Kenyatta amemtaka Naibu Rais wa Kenya ambaye anagombea Urais nchini humo, William Ruto kuacha siasa za kutukanana na kuwaambia Watu kuwa Kenyatta ana mpango wa kumuua “Hakuna haja ya matusi jameni, kila Mtu nikiwemo Mimi ana uhuru wa kupigia debe yoyote ambaye anamtaka, uamuzi utakuwa wa Wananchi”


“Nikikujibu kwasababu umesema mambo ya uongo hakuna haya ya kuwaambia Watu nataka kukuua, si mmenitusi karibu miaka mitatu, kuna Mtu amewagusa?, hiyo miaka mitatu si nimekuwa kwenye kiti (Urais) si nilikuwa na uwezo, nikiwa sina uwezo ndio niko na time ya kukutafuta?“


“Uza sera zako, achana na Mimi, nafanya kazi yangu nimalize, nyinyi kaombeni kura Wananchi wakiwapatia sawa, wakiwanyima twende nyumbani pamoja shida iko wapi?, si Dunia itaendelea?”


Itakumbukwa hivi karibuni Ruto alimwomba Kenyatta msamaha baada ya wawili hao kutofautiana mara tu baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa 2018, Kenyatta haungi mkono Ruto kuwania Urais katika uchaguzi wa Agosti na badala yake anamuunga mkono Odinga.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments