Meddie Kagere: Nilikuja kama Mfalme, Ninaondoka kama Gwiji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Aliyekua Mshambuliaji wa Simba SC Meddie Kagere amewashukuru Viongozi, Wachezaji, Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo, kwa kumuonesha upendo na kumuaga kwa heshima katika tukio maalum wakati wa Tamasha la Simba Day jana Jumapili (Agosti 08).


Kegere na Kiungo kutoka nchini Uganda Thadeo Lwanga walipata nafasi ya kipekee kuagwa na Mashabiki wa klabu ya Simba SC Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku wakitoa neno la shukurani mbele ya umma uliokua umejitokeza Uwanjani hapo.


Baada ya kukamilisha taratibu wa kuagwa, Mshambuliaji huyo kutoka nchini Rwanda aliendelea kutoa shukurani nyingine kwa Viongozi, Wachezaji na Mashabiki wa Simba SC kupitia ukurasa wake wa Instagram.


Kagere aliyejiunga na Singida Big Stars saa chache baada ya kutangazwa hatokua sehemu ya Simba SC juma lililopita ameandika: “Nilikuja kama Mfalme na sasa naondoka kama Gwji, Ahsanteni Mashabiki wote wa Simba kwa upendo wenu, Heshima kwa wachezaji wenzangu na Mashabiki kwa kuwa sehemu ya safari yangu.”


Meddie Kagere alisajiliwa Simba SC msimu wa 2017/18 akitokea Gor Mahia ya Kenya na amekua sehemu ya mafanikio ya Klabu hiyo ya Msimbazi kwa miaka minne mfululizo, huku akiibuka kinara wa kupachika mabao mara mbili mfululizo katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad