Msako wa Mifuko ya Plastiki Waanza Jiji la Dar es Salaam

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ametangaza Operesheni ya kukamata Mifuko ya Plastiki iliyokatazwa na kuwataka Wananchi kujiepusha na Matumizi ya Mifuko hiyo


RC Makalla ametangaza Operesheni hiyo wakati wa kikao kazi Wazalishaji Mifuko mbadala, Kamati ya Ulinzi na usalama na Mamlaka za Udhibiti ikiwemo TBS na NEMC Baada ya kubaini Mifuko iliyokatazwa imeanza kurudi upya.


Aidha RC Makalla ameagiza kuitishwa kikao cha Wenyeviti wa Masoko yote ya Mkoa huo na kutolewa maelekezo ya katazo la uuzaji wa Mifuko iliyokatazwa kwenye Masoko yao.


Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa Mazingira NEMC kurudi upya kutoa Elimu kwa Wananchi kuhusu Madhara ya Matumizi ya Mifuko hiyo.


Miongoni mwa Madhara ya Matumizi ya Mifuko iliyokatazwa ni Uchafuzi wa Mazingira, Ukwepaji wa Kodi* Kutokana na Mifuko Kuuzwa kinyemela pamoja na *kuua viwanda* vilivyopewa kazi ya kuzalisha Mifuko mbadala.


Kwa upande wao Mamlaka za Udhibiti kupitia Wakurugenzi wa NEMC na TBS wametumia kikao hicho kutoa tamko la kusimamia Operesheni hiyo ambapo wamemuahidi RC Makalla kuwa Operesheni hiyo itafanikiwa.


Nao Wazalishaji wa Mifuko mbadala wamekiri uzalishaji wa Mifuko iliyoruhusiwa kudorora Kutokana na kuzagaa kwa Mifuko iliyokatazwa kwenye Masoko na Maduka jambo linalopelekea viwanda vyao kufa ambapo wameiomba Serikali kusimamia Operesheni hiyo.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad