Samia ataja sababu za kumhamisha MtakaRAIS Samia Suluhu Hassan amesema Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka ni kiongozi mzuri, lakini alikuwa hatumiki vizuri Dodoma.

Alisema hayo juzi jioni wakati akisalimia wananchi wa Wanging’ombe baada ya kuwasili mkoani Njombe akitoka ziarani Mkoa wa Mbeya.

“Atanisaidia sana, maana Dodoma alikuwa anatusindikiza anatupokea, nikasema huyu kijana namtumia vibaya, ngoja nimpeleke kwenye mkoa atakapotumika sawasawa.

Kwa hiyo mtumieni ni kijana mzuri sana,” alisema Rais Samia. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa alisema Mtaka ni mbunifu, mchapakazi hivyo anaamini atafanya kazi nzuri mkoani Njombe.


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji alisema Mtaka ni jembe na Dodoma wameumia alivyohamishwa.

Dk Kijaji alimuagiza Mtaka azisimamie halmashauri ili katika asilimia nne za mikopo kwa vijana, asilimia nne kwa wanawake na asilimia mbili kwa wenye ulemavu, zitumike kujenga viwanda vya kuchakata mafuta ya parachichi kwa gharama ya kati ya Sh milioni 3.5 hadi 6.5.

Alisema katika mwaka wa fedha uliokwisha 2021/2022, Tanzania iliuza nje zaidi ya tani 40,000 za maparachichi jambo ambalo halikuwahi kutokea miaka ya nyuma.

“Mheshimiwa Rais amedhamiria kubadilisha hali ya mazao yetu hasa masoko huko nje ya nchi…ndani ya siku mbili hizi tumekuwa na mjadala wa kuona parachichi zetu kutoka Njombe, parachichi kutoka Tanzania zikiingia kwenye soko la Ulaya,” alisema Dk Kijaji.

Alisema kwa kuzingatia maelekezo ya Rais Samia wizara anayoiongoza imetengeneza mashine za kuchakata maparachichi na kwamba vijana watawezeshwa kuifanya kazi hiyo wakiwa hapo Wanging’ombe ili wawe na ajira wakiwa shambani na viwandani.

Katika mkutano huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba alihimiza kuongeza makusanyo na kusimamia mapato ili fedha zinazopatikana zitumike kutekeleza miradi ya maendeleo. “Fedha ipo, ila mkikusanya mnakula ndugu zangu, punguzeni, leteni tujenge vituo vya afya,” alisema Rais Samia

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad