Edo Kumwembe "Wachambuzi Wamejipa Kazi Nyingi Zisizo zao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


"Kuna vitu vingi huwa naacha vinipite katika mpira wetu kwa sababu sio kazi ya mchambuzi wa mpira.

Utambulisho wa jezi, Mkataba wa GSM au MO na klabu zao nakadhalika. Nadhani kazi ya mchambuzi ni kuchambua mpira kabla ya mechi, wakati wa mechi, na baada ya mechi.

Hii ndio kazi ya Pundit au analyst. Wachambuzi wetu wamejipa kazi nyingi mno. Kwa mfano, Gary Neville hawezi kupost jezi mpya za Manchester wala Arsenal. Sio kazi yake na binafsi sifanyi kwa sababu naona natangaza biashara za watu wengine.

Carragher hawezi kuzungumzia kufungiwa kwa Msemaji wala ubora wa Basi la timu...kazi hizi kule Ulaya wamepewa Waandishi nguli wa Media ambao sio wachambuzi....huku Wachambuzi wamejipa kazi nyingi za nje ya uwanja na dakika 90 za mechi hawana sana habari nazo.

Mchambuzi anachambua hadi kuchelewa kwa jezi za Simba. Ili iweje? Labda kama mtaniambia mpira wetu kivyetuvyetu. Mimi kuna mambo nayaacha yanipite. Labda itokee nimekereka mno huwa nakuja kufunga mjadala" - Edo Kumwembe.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad