Feisal Salum 'Fei Toto' Kama Mwakinyo..Awaangukia Watanzania na Kuwaomba Msamaha Kisa Taifa Stars

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kiungo mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Feisal Salum 'Fei Toto' amewaomba radhi Watanzania na mashabiki wote wa mpira kufuatia kichapo cha Stars kutoka kwa Timu ya Taifa ya Uganda.

Katika mchezo huo wa marudiano kuwania kufuzu fainali za Kombe la CHAN, ulipigwa nchini Uganda, Stars ilipigwa bao 3-0 na kuondoshwa rasmi katika michuano hiyo.

Mchezo wa kwanza uliopigwa weekendbiliyopita, Stars ilifungwa bao 1-0 na Uganda, hivyo Tanzania imeondoshwa kwa kufungwa na Uganda jumla ya bao 4-0 katika michezo miwili.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Fei Toto ameandika;

 "Watanzania wenzangu, najua inaumiza, najua inakera, najua maumivu mnayoyapitia sababu mnapenda kuiona timu yetu ya taifa ikifanya vizuri.

"Tulipewa jukumu la kuibeba bendera ya taifa letu tumewaangusha. Nichukue fursa hii kuwaomba radhi, naamini tutafanya vizuri hapo mbeleni," amesema Fei Toto.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad