Exclusive… Kajala Aanika Mazito Penzi Lake Kwa Harmonize Wameendelea Kufurahia Mapenzi Yao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Takriban miezi mitatu baada ya kurudiana na kuvishana pete ya uchumba, mastaa wawili wakubwa Bongo, Kajala Masanja na Harmonize wameendelea kufurahia mapenzi yao.

Harmonize au Harmo na Kajala walirudiana mwezi Mei mwaka huu baada ya kutengana katika hali tatanishi tangu mwezi Aprili, mwaka jana.

Miezi mitano iliyopita Harmonize alimtema mlimbwende wa Australia aliyekuwa mpenzi wake aitwaye Briana Jai na kuanza juhudi za kufufua penzi lake na Kajala au Mama Pau.

Harmonize alikiri mbele ya gazeti hili la IJUMAA kuwa hisia zake kwa Kajala bado zilikuwa hai na alikuwa hana hisia hata tone kwa Briana.

Kufuatia hatua hiyo, alianza kutia bidii ya kumrejesha Kajala na hatimaye akafanikiwa.

AKIRI MAPENZI KUZIDI MARADUFU

Sasa; akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Kajala mwenye umri wa miaka 39 anakiri kuwa mapenzi yake kwa Harmonize yamezidi maradufu kadiri siku zinavyosonga.

Kajala ambaye kwa sasa siyo mchumba wa Harmonize tu, bali pia ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya usimamizi ya Lebo ya Konde Music Worldwide anafunguka siri ya kuongezeka kwa mahaba yake kwa jamaa huyo.

Kajala alianza rasmi kazi yake ndani ya Konde Gang miezi miwili iliyopita baada ya Harmonize kumpa wadhifa huo.

SIRI NI MAZOEZI

Kajala ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, siri ya jambo hili ni kutokana na mazoezi wanayofanya yeye na mpenzi wake huyo ambayo anahisi yanaongeza mahaba kila siku.

Kajala anasema kuwa, mtu ukiwa unafanya mazoezi na mpenzi wako ni kitu kimoja kizuri mno kwani inaongeza ukaribu miongoni mwa wapenzi.

Anasema kuwa, mazoezi ya pamoja kwa wapenzi yanakuwa ndiyo maisha yenu ya kila siku.

Kajala anasema kuwa, kubwa zaidi mahaba yanaongezeka kwa sababu mnapata muda mrefu wa kuwa pamoja na kutaniana.

“Asikwambie mtu, kufanya mazoezi na mpenzi wako yanafanya mahaba yanaongezeka sana na mnapata muda mwingi wa kuzoeana sana na kufurahia kila sekunde ya uhusiano wenu,” anasema Kajala na kuongeza

KAJALA: WAPENZI WATANOGEWA

“Kila mtu anaweza kujiuliza ni lini alifanya mazoezi na mpenzi wake? Na je, baada ya mazoezi walijisikiaje?

“Mazoezi ya aina yoyote hata kama siyo ya gym kama kukimbia pamoja yana namna f’lani yanaweza kuwaondolea hata ugomvi baina yenu na kujikuta mkichangamka na kusahau changamoto zenu kisha mkanogewa.”

Kajala anawashauri wanandoa, wachumba au wapenzi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi hata kwa nusu saa tu kwa siku ambapo wataona mabadiliko kwenye mapenzi yao.

Hivi karibuni, Kajala alishindwa kuzuilia furaha yake baada ya Harmonize kumzawadia mkufu wa bei mbaya.

Harmonize au Konde Boy alimkabidhi Kajala zawadi hiyo wakati wakiadhimisha mizei miwili ya uchumba wao.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad