Fisi Aua Mbuzi 10 na Kujeruhi 9 Chato

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mbuzi 10 wamekufa na wengine 9 kujeruhiwa baada ya kuvamiwa na kundi la Fisi usiku wa kuamkia leo Septemba 23, 2022, kwenye zizi la Masunbuko Shirungu mkazi wa Kijiji cha Itale wilayani Chato mkoani Geita na baadae Fisi huyo aliuawa na Mbwa wa mfugaji.


Afisa Mifugo na Uvuvi wilaya Chato Dokta Elfas Msenya, ameeleza hasara iliyojitokeza kwa nfugaji huyo.

"Mbuzi 1 kwa sasa wastani wa bei ni shilingi  90,000 zidisha mara idadi ya mifugo iliyoathirika utaona hasara ilivyokubwa", amesema Msenya.

Aidha Msenya anaelezea hatua za awali walizochukua kuhakikisha mifugo minginge haikumbani cha changamoto ya kuliwa na Fisi.


"Hatua za haraka tukizochukua kwa sasa, tumewashauri kuimarisha mabanda yao au wajenge mabanda imara bila kusahau kuimarisha ulinzi hasa nyakati za usiku lakini pia kutowafuata wanyama wakali kwenye makazi yao na waache kujenga karibu na maeneo ya mapori,".

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad