Hivi Ndivyo Mwanafunzi Alivyomuua Mwenzake Baada ya Kushindwa Kumbaka Chumbani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 




Mwanafunzi Faraja Kasole (16) wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Sinde Jijini Mbeya, ameuawa kwa kukatwa na shoka shingoni na Mwanafunzi mwenzie aitwaye Humphrey Ngogo ( 17) ambaye anasoma kidato cha tano Shule ya Sekondari Iduda baada ya kushindwa kumbaka.


Kamanda wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema chanzo cha mauaji ni tamaa za kimwili ambapo Mtuhumiwa alifanya jaribio la kumbaka Faraja lakini baada ya kuzidiwa nguvu akachukua shoka na kumpiga nalo kichwani.


“Kabla ya tukio hilo, Mtuhumiwa alifika nyumbani kwa Marehemu ambaye kwa muda huo alikuwa peke yake na kisha kumvamia chumbani kwake kwa nia ya kumbaka na alipozidiwa nguvu ndipo alimua kuchukua shoka na kumpiga nalo”


Kamanda Matei amesema upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa Mahakamani kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria ikiwamo Mtuhumiwa kuchukuliwa hatua.


“Jeshi la Polisi linalaani tukio hili kikatili na linatoa pole kwa Wazazi na Familia ya Marehemu, hata hivyo tunatoa rai kwa Wazazi au walezi kujenga tabia ya kuzungumza na Watoto wao kuhusu masuala ya makuzi na kujali zaidi masomo na kuachana na tama za kimapenzi wangali masomoni ili kujiepusha na matukio kama hayo,”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad