Mashabiki Simba waiteka Malawi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Mashabiki wa Simba kutoka Tanzania wamewasili jijini Lilongwe tayari kwa kuisapoti timu yao inayocheza dhidi ya Big Bullet.
Lilongwe. Mashabiki wa Simba kutoka Tanzania leo wameuteka mtaa wa Divo uliopo jijini hapa nchini Malawi huku wakisisitiza kuwa lazima leo Nyasa Big Bullet alale 3-0.

Simba inatarajia kushuka uwanjani saa 9:00 alasiri kwa saa za Malawi kupepetana na wapinzani wake ambao ni wenyeji kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi itakayopigwa uwanja wa Taifa Bingu.

Leo mashabiki wa Wekundu hao wametua kwa mzuka mwingi na kupokelewa na wenyeji wao na kufanya mtaa huo kuzizima kwa muda kutokana na 'vibe' walilokuwa nalo.

View this post on Instagram
A post shared by Mwanaspoti (@mwanaspoti_tz)


Wakizungumza na Mwanaspoti wamesema wameamua kuifuata timu yao kuhakikisha wanaipa sapoti na kuondoka na ushindi mnono licha ya kuwa ugenini.

Amiri Mrisho mmoja wa mashabiki amesema leo wanaamini Chama lao litaibuka na ushindi wa mabao matatu kutokana na uwezo wa kikosi na mchezaji mmoja mmoja.

Naye Rehema Peter amesema hawana wasiwasi na Mnyama na lazima wapinzani wale nyingi kutokana na nguvu waliyonayo.


"Tumekuja kuwaua, yeyote atafunga hata Banda (Peter) anaweza kumaliza mchezo leo tunachotaka ni ushindi, tumejipanga." amesema Rehema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad