Masharti Mazito Utajiri wa Mondi… Siri Yafichuka Kutosadia Ndugu Zake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


NASIBU Abdul Jumaa almaarufu Diamond Platnumz; ni staa mkubwa wa muziki wa kimataifa wa Tanzania ambaye mitandao kedekede inamtaja kuwa ndiye msanii tajiri zaidi kwa Tanzania na ukanda mzima wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2022, lakini nyuma ya pazia kuna masharti mazito juu ya utajiri huo, IJUMAA limedokezwa.

Utajiri wa Diamond au Mondi unatajwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni 20 za Kitanzania kwa mujibu wa ripoti mbalimbali barani Afrika.

Ripoti ya Mtandao wa Forbes Africa ya mwaka 2022 inamtaja Diamond na Rayvanny kuwa ndiyo wasanii wenye mafanikio zaidi Afrika Mashariki.

MANUNG’UNIKO KUTOSAIDIA NDUGU

Lakini pamoja na utajiri huo, uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA umebaini kuwa, kuna manung’uniko ya chinichini miongoni mwa wanafamilia kwamba, Diamond au Simba kama kweli ni tajiri kiasi hicho ni kwa nini hasaidii ndugu zake?

MAMA DANGOTE

Ukimuacha mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote ambaye inasemekana Mondi anammwagia pesa atakavyo, wapo ndugu zake wa damu na familia ambao maisha yao yanatia huruma na mtu huwezi kuamini kama ni ndugu zake au wana uhusiano wowote ule.

ESMA PLATNUMZ

Mmoja wa ndugu wa damu wa Diamond ni Esma Khan almaarufu Esma Platnumz; huyu ni mjasiriamali wa vitenge ambaye wanashea mama ambaye ni Mama Dangote, lakini baba ni tofauti.

Baada ya kusikia madai ya Diamond kutosaidia ndugu na kwamba yeye (Esma) anaishi nyumba ya kupanga na hana gari, anasema kuwa, yeye hajawahi na wala haishi kwa kutegemea pesa za Diamond kama ambavyo mama yake anafaidi.

RICARDO MOMO NA IDDY SANTOS

Ndugu wengine wa Diamond ni Ricardo Momo na Iddy Santos; hawa ni wafanyakazi wa kawaida ndani ya Taasisi ya Wasafi inayomilikiwa na Diamond ambao ameshea nao baba aitwaye Salum Nyange, lakini inasemekana hawaishi maisha ya kifahari kuendana na Diamond.

ROMMY JONS

Ndugu mwingine wa Diamond ni Romy Jons; huyu ni DJ wake rasmi ambaye humtambulisha kama kaka yake kwani wamekua wote tangu utotoni, lakini ni mtoto wa mama yake mdogo aitwaye Shani.

Hivi karibuni, Romy Jons aliibua gumzo kwenye mitandao na kulazimika kumjibu shabiki ambaye alimshangaa kwa kumwambia kwamba yeye anajishughulisha na biashara ya matangazo ya waganga wa kienyeji kwa malipo duni ilihali ndugu yake ambaye ni Diamond ana pesa kiasi cha kumiliki ndege aina ya helikopta na ananukia utajiri.

Kauli ya shabiki huyo iliungwa mkono na wafuasi wengi wakisema kuwa hakukosea kusema kwamba Romy Jons anafanya matangazo ya waganga wa kienyeji kwani ndiyo ukweli mtupu huo.

Maoni hayo yalimfikia Riomy Jons kwa mshtuko ambapo ililazimu kwa uchungu huku akidokeza kwamba mashabiki wengine hawaridhiki na wanamchanganya kwani ni haohao walimuambia kwamba ajitegemee na kuacha kutegemea vya nduguye.

“Jamani si mmeniambia nisitegemee cha ndugu kuwa nitakufa maskini, mbona mnanichanganya sasa?” Romy Jons alijibu kwa uchungu.

QUEEN DARLEEN

Awali kabla ya Mama Dangote kuanika ukweli, wengi walijua kwamba, msanii Queen Darleen ni msanii na ndugu wa damu wa Diamond wanayeshea baba mmoja ambaye ni Mzee Abdul.

Hata hivyo, baada ya Mama Dangote kumwaga mchele, Queen Darleen ameendelea kubaki chini ya Lebo ya WCB ya Diamond kwani walikua pamoja wakiamini wote baba yao ni Mzee Abdul kumbe sivyo!

Watu wa karibu wanasema kuwa, pamoja na ukweli huo, lakini maisha ya Queen Darleen hayasadifu ukaribu wake na Diamond hata kama ni wa kimalezi.

MZEE ABDUL

Mzee Abdul; ni baba mlezi wa Diamond ambaye anatumia jina lake mpaka leo kwenye makabrasha yake rasmi ya kiserikali na hata kitambulisho cha Nida.

Awali, Mzee Abdul alifahamika kama baba mzazi wa Diamond akiitwa Baba D, kabla ya Mama Dangote kumtaja Salum Nyange kuwa baba mzazi wa Diamond.

Watu wanadai kuwa, maisha anayoishi Mzee Abdul hayasadifu ukaribu na Diamond hata kama alimtelekeza kwani hivi karibuni aliripotiwa hali yake siyo nzuri akisumbuliwa na kansa ya ngozi, lakini haijasikika kama Diamond amemsaidia.

MWIJAKU: DIAMOND HANA PESA

Mtangazaji Mwijaku anasema kuwa, kitendo cha Diamond kushindwa kusaidia ndugu zake ndicho kinathibitisha kwamba, jamaa huyo si tajiri kama ambavyo watu wanaaminishwa.

“Diamond hana pesa, angekuwa na pesa angeshindwa kuwasaidia ndugu zake? Yule Ricardo Momo (kaka wa Diamond) ana maisha magumu sana, kama huyo Diamond ana pesa kwa nini asimsaidie ndugu yake?” Anahoji Mwijaku.

PESA ZA MASHARTI?

Baadhi ya watu wanadai kuwa, ukiwachunguza watu wengi wanaoaminika ni matajiri, basi huwa hawawasaidii ndugu zao kutokana na masharti f’lanif’lani wanayokuwa wamepewa ili kuutunza utajiri huo.

Madai mazito yanayotolewa na wenye kuamini mambo hayo ni kwamba, kwa muda mrefu Diamond amekuwa akihusishwa na jamii ya siri ya Freemason ambayo inaaminika huwapa watu utajiri wa masharti kama hayo na kutoa kafara.

Stori; MWANDISHI WETU, Dar

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad