Mjamzito abakwa hadi kufariki “Mbakaji alimvunja shingo”

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mkazi wa Manispaa, Mohamed Njali, kwa tuhuma za kumdhalilisha kijinsia mama mjamzito, Atka Kivenule na kumsababishia kifo chake.

Tukio hilo limetokea Jumamosi usiku mtaa wa Maweni, kata ya Kitazini/Myomboni ambapo mtuhumiwa huyo alivamia nyumbani kwa Adeline Kileo, saa 5 usiku.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Allan Bukumbi, alikiri kutokea kwa tukio hilo na wanaendelea na uchunguzi ili kujua sababu za mauaji hayo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Alfred Mwakalebela amethibitisha kupokea mwili wa mwanamke anayedaiwa kubakwa hadi kufariki akiwa na ujauzito wa wiki 10.

“Inasemekana alikuwa amelala ndani akavamiwa na mtu na katika uchunguzi tumegundua alivunjwa koromeo tulikuta michubuko inaonekana mbakaji alikuwa akimnyonga shingo ili atimize azma yake,’ Mwakalebela.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amethibitisha kutokea tukio hilo na kwamba, uchunguzi zaidi unaendelea.6
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad