R-Kelly Akutwa na Kesi ya Unyanyasaji wa Watoto Kingono

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


NYOTA wa R&B mwenye umri wa miaka 55 nchini Marekani, R-Kelly amepatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono wa watoto katika kesi ya pili iliyoendeshwa na mahakama ya shirikisho.

Jopo la mahakama lilimkuta R-Kelly na hatia ya makosa sita kati ya 13 katika kesi ya wiki nne iliyoendeshwa katika mji wa Chicago, ambapo msanii huyo ndipo anapoishi.

Mahakama ilimuondolea kesi ya jimbo ambayo ilipaswa kubaini iwapo kuna ushahidi kuhusu mashitaka ya ponografia ya watoto katika mwaka 2008.

Mwaka jana muimbaji huyo wa Bump n’ Grind alipatikana na hatia ya usafirishaji haramu wa watu kwa ajili ya ngono na kuhusika na njama za wizi na ulaghai mjini New York, ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

R-Kelly ambaye jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly, alipatikana Jumatano na hatia tatu za kuwalaghai watoto kwa ajili ya ngono na makosa matatu ya kutengeneza picha za ngono za watoto.

Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad