Watuhumiwa 38 wakamatwa Arusha, mmoja akutwa akisafirisha dawa za kulevya kwa kutumia lori la Mafuta.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 38 wanaojihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu ambapo kati yao mmoja amekutwa akiwa anasafirisha madawa ya kulevya aina ya mirungi kwa kutumia gari la kubeba mafuta.

Akitoa taarifa hiyo leo Septemba 11, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika operesheni iliyofanyika kuanzia Septemba 05 hadi Septemba 10, 2022 ikiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Arusha kwa lengo la kuwasaka watuhumiwa wa uhalifu.

Kamanda Masejo amesema kuwa tarehe 10.09.2022 muda wa saa 12:30 asubuhi huko katika mtaa wa Kikwe uliopo katika kata ya Kikwe wilayani Arumeru, Jeshi hilo la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Allen Wilbard Kasamu (49) dereva na mkazi wa Suye Jijini Arusha akiwa anasafirisha madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni mirungi yenye uzito wa zaidi ya robo tani ambao ni kilo 390.75kg.

Amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa anasafirisha madawa hayo ya kulevya kwa kutumia gari aina ya Mitsubish Canter – Tanker ambalo ni maalumu kwa ajili ya kubeba mafuta ambapo alitumia mbinu za kupakia ndani ya tenki la mafuta ili asijulikane.


Sambamba na hilo pia katika operesheni hiyo walifanikiwa kukamata pikipiki 13 zilizokua zinatumika katika matukio ya uhalifu, gongo lita 08, bangi yenye uzito wa kilo 70 pamoja na laptop 03.

Hata hivyo Kamanda Masejo amesema kuwa hadi hivi sasa jeshi la Polisi mkoani humo bado linaendelea na upelelezi ikiwemo kuwahoji watuhumiwa hao na pindi upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya kutolewa maamuzi.

Ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Sambamba na hilo pia amewataka baadhi ya watu wachache wanaojihusisha na uhalifu hususani biashara ya dawa za kulevya kuacha mara moja kwani wataendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua.

Katika hatua nyingine Kamanda Masejo amesema kwa Mkoa wa Arusha wananchi wameanza kujitokeza kusalimisha silaha zao katika vituo vya polisi na kutoa rai kwa watu ambao wanamiliki silaha kinyume cha Sheria kufika katika vituo vya Polisi ama ofisi za watendaji wa mitaa kusalimisha silaha hizo katika kipindi hiki ambacho Serikali imetoa msamaha kwa ambao watasalimisha.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad