Mastaa Waliotokana na Mashindano ya Umiss Bongo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Bongo ‘mastaa’ wa kike ni wengi na kila mmoja anaIjua mwenyewe njia aliyoitumia hadi kupata jina mjini, wapo waliopata umaarufu kwa sifa nzuri na wapo wale wa tofauti.

Leo hii nataka usanuke kuwa, mastaa wengi wa kike Bongo wametoka kwenye mashindano ya umiss hapa Tanzania.

Tukirudi kwenye Masijala za hawa ‘mastaa’ wetu wakike, tutakumbuka walipotokakwa. Kwa kuanza tuanze na binti Sepetu ambae dunia inamjua kama miss Tanzania 2006.

Katika kinyang’anyiro cha umiss mwaka huo kulikuwa na warembo wengine kama vile Jokate alishika namba 2, Lisa Poulsen namba 3, Uwoya namba 5 na Aunty Eziekeil ambaye hakubahatika hata kunusa top 10.

Mwaka uliofuata 2007, katika mashindano ya miss Mwanza alipatikana staa mwingine Zamaradi Mketema, ambae kipindi hicho Uwoya na Jokate wakiwa ni miongoni mwa majaji katika mashindano hayo.

Wifi yetu/Shemeji yetu kwa #ReyKigosi, hapa namzungumzia Chuchu Hansi ambae yupo vizuri kwenye filamu zetu za hapa Bongo pia alikuwa Miss Tanga 2005.

Warembo wengi waliendelea kujikuta wanafika mjini baada ya kutoka kwenye umiss, Lulu Abbas a.k.a Lulu Diva pia ni Miss Pwani namba 2 na Miss Kibaha 2013. Hamisa Mobeto nae alikuwa Miss Dar Indian Ocean namba mbili 2011 na akashiriki Miss Tz mwaka huo huo, lakini alitoka patupu. Hakukata tamaa 2012 Misa alishiriki Miss University Africa na kuingia top 10.

Wengi wao waliangukia kwenye #BongoMuvi, na miaka ya sasa tunawaona wanaanza kujitafuta kwenye muziki kama vile Flora Mvungi yeye alikuwa Miss Pwani na Miss Kanda ya Mashariki 2008, bila ya kumsahau Jini kabula ni Miss Kariakoo wa miaka ya nyuma ingawa hakutoboa Miss Tanzania taifa.

Aliyekuwa mke wa Reginald Mengi, Jacqueline Mengi ni miss Tanzania 2000, kuna Balozi Hoyce Temu Miss Tanzania 1999, bila kumsahau Rashida Wanjara ni Miss Mara, Miss Kanda ya Ziwa na Top Model Miss Tanzania 2002.

Warembo wote hawa wanafanya vizuri hadi kesho, bado wanatajwa nje na ndani ya Tanzania.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad