Mchungaji Dar Adaiwa Kumtorosha Mke wa Muumini, Ampangishia Nyumba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mchungaji Edwin Taji wa Kanisa la Anglicana, Yombo Kiwalani jijini Dar es Salaam anadaiwa kusimamishwa kutoa huduma ya kichungaji baada ya kudaiwa kumtorosha mke wa muumini wake na kumpangishia nyumba eneo la Pugu Kajiungeni.

Madai dhidi ya mchungaji huyo yalitolewa na muumini wa kanisa hilo, Simon Ngalawa mkazi wa Yombo Kiwalani akilalamika kuwa mkewe Ester Makunya anajihusisha kimapenzi na mchungaji Tija.

Ngalawa anadai baada ya kupata tetesi hizo kutoka kwa waumini na ndugu zake, alibaini kuwa mkewe alianza kuwa na fedha wakati hafanyi kazi wala biashara, na kwamba baada ya kupitia kipindi kigumu cha maisha ndipo alipoondoka nyumbani miaka mitatu iliyopita na kuishi Kiwalani ambako inadaiwa alipangishiwa nyumba na kufunguliwa duka na mchungaji huyo.

Ameongeza kuwa licha ya kuitisha vikao vya familia, kwenda Ustawi wa Jamii na Polisi kweye Dawati la Jinsia, lakini imeshindikana kwa mkewe kurudi nyumbani, na ndipo alipokutana na viongozi wa juu wa kanisa hilo ili kumshitaki mchungaji huyo.


Taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo zinaeleza kuwa mchungaji Tija amesimamishwa wiki mbili zilizopita huku shauri lake likiendelea kujadiliwa na wakuu wa kanisa hilo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad