Meneja wa Diamond Platnumz Babu Tale Atangaza Kuwalipia Tickets za Ndege Wasanii 7 Waliotajwa Kuwania Tuzo za Afrimma Kutoka Tanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mbunge wa Morogoro Mashariki na Meneja wa Wasanii wa muziki chini ya lebo ya @wcb_wasafi Hamisi Taletale @babutale ameainisha dhamira yake ya kupambania tickets 7 za kuwafikisha Nchini Marekani Wasanii 7 wa Tanzania waliotajwa kuwania tuzo hizo mwaka huu kwa lengo la kuleta matokeo chanya kwenye ukuaji wa muziki na Tasnia kwa ujumla.

Tale pia ameliomba Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kushughulikia upande wa VISA kwa Wasanii hao kwani tayari wana barua za mialiko kushiriki katika hafla ya utoaji wa Tuzo hizo.

Tale ameandika -“Kwa sasa Muziki wetu umekua na kuifikia Dunia, ndio maana Wasanii wetu wameendelea kuchaguliwa kuwania tuzo mbali mbali kubwa ikiwepo hizi tuzo za AFIMMA @afrimma .

Tuzo hizi zitafanyika nchini Marekani mwaka huu 2022. Kwa kutambua umuhimu wa kuwakilisha nchi yetu, uwepo wangu kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu na dhima ya kukuza sanaa yetu, nadhamiria kuhangaikia tiketi Saba za Wasanii waliochaguliwa kuwania tuzo hizi. NB: Hatakaewahi kupata VISA ndiye atakaewahi kupata ticket.

Hivyo niombe Baraza la Sanaa Tanzania @basata.tanzania (BASATA), kusaidia upatikanaji wa VISA za Wasanii waliochaguliwa kwani wote wanabarua za mwaliko.

Tuzo hizi ni muhimu kwa ukuaji wa muziki wetu na kulitangaza Taifa letu kwenye kile alichokianzisha Mheshimiwa Rais wetu cha kuvuta watalii nchini. Hii ikawe sehemu ya kila msanii shiriki kuizungumzia Royal tour akiwa huko nchini Marekani”

Mtazamo wako ni upi kwenye hili la @babutale!? Share na sisi keenye uwanja wa comments! • 

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad