Rais wa Kenya William Ruto Aomba Nchi za Afrika Mashariki Kusiwe na Mipaka ya Nchi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais wa Kenya William Ruto amemuomba Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akiwa kama Mzee miongoni mwa Viongozi wa Afrika Mashariki kupambana ili kuhakikisha mipaka inayotenganisha Nchi inaondolewa na kuondoa vikwazo vingine vyote ili Nchi za Jumuiya za Afrika Mashariki zisitenganishwe na mipaka na kuwe na urahisi wa muingiliano wa Watu na biashara zao.


Rais Ruto ametoa ombi hilo mbele ya Museveni leo Uganda wakati akiongea katika sherehe za kutimiza miaka 60 tangu Uganda ilipojipatia Uhuru kutoka kwa Waingereza.


“Mzee wetu Museveni una changamoto hiyo ya kutuongoza ili kuhakikisha tunaiangusha mipaka iliyoyopo na kuwe na soko huru, Wana Afrika Mashariki hatuwezi kugawana njaa au umasikini lakini tunaweza kugawana fursa na ustawi wetu, mipaka imekuwa kikwazo tuigeuze kuwa Daraja ili Watu wasafiri na bidhaa zisafirishwe kutoka Nchi moja kwenda nyingine bila masharti”


Kauli ya Ruto inakuja siku chache tangu aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Ardhini la Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye ni Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, aseme mipaka iliyopo iliwekwa na Wakoloni na hakuna haja ya kuendelea kuiacha badala yake Nchi za Afrika Mashariki zinapaswa kuifuta mipaka hiyo na kutengeneza Taifa moja.


Mtoto huyo wa Museveni alienda mbali zaidi na kusema ameongea na Baba yake (Rais Museveni) na kumueleza kwamba Vijana wa Afrika Mashariki wameamua Nchi za Afrika Mashariki ziungane na kuwa Taifa moja.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad