Serengeti Girls yatakata Kombe la Dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




TIMU ya Taifa Tanzania chini ya miaka 17 upande wa Wanawake 'Serengeti Boys' imepata ushindi wa kwanza baada ya kuifunga 2-1 Ufaransa katika Fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini India.
 

View this post on Instagram
A post shared by Mwananchi (@mwananchi_official)


Serengeti ambayo ipo kundi D imepata pointi tatu za kwanza, huku mchezo wa kwanza ikifungwa 4-0 na Japan.

Mabao ya Diana Mnally na Christer John yalitosha kuifanya Serengeti Girls itoke kifua mbele kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Katika mchezo huo kiungo wa Serengeti Girls, Joyce Lema alionyeshewa kadi nyekundu baada ya kuonyeshewa kadi mbili hali itakayomfanya akose mchezo ujao.

Serengeti itashuka tena uwanjani dhidi ya Canada Oktoba 18 mchezo ambao wanahitaji ushindi ili kuwa katika uhakika wa kusonga mbele zaidi katika hatua ya mtoano.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad