Talaka ya Anerlisa na Ben Pol Yatoka, Sio Mume na Mke Tena...Anerlisa Afunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ni rasmi kuwa mfanyabiashara wa Kenya Anerlisa Muigai na mwimbaji wa R'n'b kutoka Tanzania Ben Pol sio mke na mume tena. Anerlisa na Ben Pol walifunga ndoa Mei 2020 katika Kanisa Katoliki la St Gaspar huko Mbezi Beach, Tanzania lakini wakatengana mwaka jana. Baada ya kutengana, Ben aliwasilisha kesi ya talaka mahakamani.

Katika chapisho kwenye Instagram, Anerlisa ambaye ni binti wa seneta wa Nakuru Tabitha Karanja amefichua kuwa talaka yake na mwimbaji huyo wa Bongo hatimaye imekamilika.

Anerlisa amewashukuru mawakili wake kwa kuhakikisha kuwa mchakato wa talaka yake umekamilika

“Niko huru rasmi. Haitakuwa sawa kutowatambua mawakili hawa wawili ambao walifanya kazi bila kuchoka kuhakikisha kwamba talaka inafanywa haraka na sio kusubiri kwa miaka. Hamza Jabir na Hosea Chamba, asanteni kwa kazi zenu na kwa kufanya kila kitu mlivyoombwa.” alisema kwenye Insta stori.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad