VIDEO: Wacheza Sarakasi Kutoka Tanzania Watisha Australia’s Got Talent, Waibuka Washindi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wasanii wawili wa sarakasi kutoka Tanzania Ibrahim na Fadhili Ramdhan wanaounda kundi la The Ramadhan Brothers wamefanikiwa kuibuka Washindi wa hatua ya kwanza kwenye shindano la Australia’s Got Talent mwaka 2022 na sasa wataendelea kwenye hatua inayofuata ya Shindano hilo.


Hii ni mara ya kwanza kwao kufika Australia na mara ya kwanza kwao kufanya onesho la sarakasi kwenye show kubwa ya TV ambapo ubunifu wao uliibuka kivutio kikubwa kwa Watazamaji na Majaji akiwemo Jaji mmoja ambaye alikiri kuifahamu Tanzania na kusema amewahi kufika Mlima Kilimanjaro.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI:

Kwa mujibu wa Jaji wa Shindano zawadi kwa shindano hilo ni USD 100,000 (Tsh. Milioni 230) ambazo wamesema wakizipata watazitumia kuwainua Vijana wenzao wa Afrika wenye ndoto za kufikia mafanikio na kuna Shule ya vipaji ambayo wataisaidia.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad