Watatu wafariki dunia Kilwa kwa kula kasa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



WATU watatu akiwemo mtoto mwenye umri wa mwezi mmoja wakazi wa kijiji cha Rushungi wilayani Kilwa mkoani Lindi wamefariki dunia baada ya kula samaki aina ya Kasa-ng’amba ambaye aliokotwa ufukweni mwa bahari. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Lindi jana tarehe 10 Oktoba, 2022, Mganga Mkuu mkoa huo, Dk. Kheri Kagya amesema tarehe 5 Oktoba, 2022 Zahanati ya Rushungi iliwapokea watu waliokula samaki huyo wakiwa na matatizo ya kuhara, kulegea mwili na wengine kupoteza fahamu na mtoto mmoja alifariki katika zahanati hiyo.

Dk. Kagya amesema hadi kufikia asubuhi tarehe 9 Oktoba, 2022 watu waliofika zahanati ya Rushungi walikuwa 33 na kati ya hao 13 walipewa rufaa kwenda kituo cha afya Kitomanga manispaa ya Lindi.


Amesema baadae watu watatu ambao ni wanaume hali zao zilikuwa mbaya zaidi na kupewa rufaa hadi hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine.


Ameongeza kuwa watu hao watatu waliopewa rufaa kwenda Sokoine, wawili wamefariki dunia ambao ni mwanaume mwenye umri wa miaka 41 na mtoto mwenye umri wa miaka 8 huku mmoja akiendelea na matibabu katika chumba cha uangalizi maalum.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad