Media za Tanzania Zina Mpango wa Kuuwa Bongo Flava....?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kwanini kila siku Tuzungumzie issue moja? Hivi Media zetu zina mpango wa kupoteza Wasanii wa Tanzania au?

Jana usiku baada ya Umeme kukatwa Kuna redio moja kubwa tu nimesikiliza Kwa Saa Zima, Nyimbo za kibongo Zilipigwa tatu tu, zilizobaki ni Amapiano na Afrobeats. ZIMEPIGWA AMAPIANO MPAKA NIKAJUA NIKO SOUTH, NIKAAMUA KUTOKA NJE NIANGALIE NIPO WAPI, KUTOKA NJE NAJIKUTA NIPO UBUNGO.

Inauma sana!, Hivi Tanzania hakuna wasanii wenye ngoma kali ambazo zinatakiwa kupigwa redioni?

Mbona Ma-DJ na Music Departments za Media za Bongo mnashobo sana na Nyimbo za Nje? Hivi mnajua kwamba Nigeria na South kuna Sera kabisa za Muziki na Wanapiga kazi za Ndani kwa zaidi ya Asilimia 70!

Kwanini sisi hatutaki Mabadiliko? Aliyeturoga ameshafariki au?

Hivi Taifa linapata faida gani baada ya nyie kupiga nyimbo za Nigeria na south?

Ombeni nisipate madaraka nitanyoosha watu, Lazima Tuweke mipango ya Muziki wa kitanzania na Wanamuziki wa Tanzania kuwa namba moja Afrika. Nigeria na South wao ni kina nani? Wana damu za Blue au?

By Hopetyga
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad