Wanafunzi wanne wadhalilishwa kingono, 25 waondoka shuleni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



WANAFUNZI 25 wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Spring Valley Mkoani Iringa wanadaiwa kuondoka shuleni hapo na kugoma kurudi kutokana na wenzao wanne kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa kingono vinavyodaiwa kufanywa na Meneja wa Shule hiyo.
Inadaiwa siku ya jumamosi waliandamana kwenda katika kituo cha polisi kutoa taarifa na baadaye dawati la jinsia kulazimika kuwapeleka katika Sekondari ya Lugalo iliyopo Manispa ya Iringa.

Mwalimu wa Malezi Lugalo Hawa Kibona amethibitisha kupelekwa kwa watoto hao jumamosi jioni ya saa12 na kupewa hifadhi.

Akiongea kwa njia ya simu Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya iringa Tiniel Mbaga, amesema watoto hao wamekuwa wakipokea vitisho vya kufukuzwa Shule kutoka kwa Meneja na hivyo wakaamua kuondoka Shuleni hapo.

Meneja wa Shule pamoja na Mkuu wa Shule wamechukuliwa na Polisi huku Wanafunzi hao wakiendelea kuwepo Lugalo na mustakabali wao utajulikana leo Jumatatu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad