Bondia Mwakinyo Kuchunguzwa Sakata la Kupoteza Pambano Nchini Uingereza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amesema wizara bado inaendelea kuchunguza sakata la Hassan Mwakinyo baada ya kupoteza pambano lake nchini Uingereza.



Mchengerwa amesema wamekuwa na utaratibu wa kufuatilia kila jambo linalotokea katika sekta ya Sanaa, Utamaduni na Michezo hivyo walipoona sintofahamu iliyotokea nchini Uingereza wameedelea kufuatilia kjua nini kilitokea.


“Nimefanya mazungumzo nilipokuwa kule Tanga na Mwakinyo, tumekubaliana tuonane ili tuweze kujua hasa kiundani kile ambacho kilitokea. Lakini pia hata yeye ana madai yake kadhaa ambayo aliniambia anatamani kuniona ili tuweze kuzumza,” amesema Waziri Mohammed Mchengerwa


Aidha, amesema kama wizara iliyopewa dhamana ya kusimamia michezo hawachukulii jambo lolote kawaida, jukumu lao ni kuhakikisha wanafuatilia kila jambo ambalo haliko sawa linalotokea ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuwa ni nchi ndiyo inayowakilishwa.


Septemba 18, 2022 Bodi ya Ngumi za Kulipwa Uingereza (BBBC) lilimfungia bondia Hassan Mwakinyo kucheza ngumi nchini Uingereza siku chache baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Liam Smith kwa TKO raundi ya nne katika pambano lenye raundi 12 na kudai sababu za kupoteza mchezo huo ni baada ya kupoteza begi lake na kupewa viatu ambavyo havikumfaa.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad