Bosi mpya Simba Atoa Neno, Amtaja Barbara Ukumbini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bosi mpya Simba Atoa Neno, Amtaja Barbara Ukumbini


Ofisa Mtendaji Mkuu mpya wa Simba, Imani Kajula amesema mtangulizi wake, Barbara Gonzalez bado hajaondoka kwenye klabu hiyo na wanaendelea kushirikiana.


Akizungumza mbele ya Wanachama waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa kawaida wa klabu unaokwenda sanjari na chaguzi mkuu hii leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Kajula amesema Barbara ataendelea kuwa mtu muhimu kwao.


"Jana niliwasiliana naye na Jumatano tumepanga kukutana ili kujadili mambo mbalimbali, lengo ni kuhakikisha tunapiga hatua zaidi."


Kajula aliteuliwa Januari 26, mwaka huu alichukua nafasi ya Barbara Gonzalez aliyejiuzulu Disemba 10 mwaka jana.


Kajula ni mwanachama wa muda mrefu wa Simba na mbobezi katika masuala ya Kibenki na masoko akiwa na uzoefu wa kutosha aliouvuna akihudumu katika taasisi mbalimbali.


Pia ni mzoefu kwenye masuala ya uongozi wa mpira kwani alikuwepo kwenye Kamati ya Maandalizi ya Michuano ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) iliyofanyika nchini mwaka 2019.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad