Ticker

6/recent/ticker-posts

Chama Avunja Ukimya Atoa Tamko Zito Simba

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPAKiungo wa Klabu ya Simba Clatous Chama

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amesema kuwa kwake ambacho anakiangalia ni kuona timu inapata mafanikio kisha mengine yatafuta na wala sio ya muhimu zaidi kama timu kupata ushindi.

Chama katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City ukiwa ni wa Ligi Kuu Bara alitolewa katika dakika ya 32 ya mchezo ambapo Simba katika mchezo huo walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Kitendo hicho kiliwakasirisha mashabiki wa timu hiyo kwa madai kuwa hakustahili kutolewa kwani alikuwa anacheza vizuri na kabla hajatolewa alitoa asisti kwa Saidi Ntibazonkiza.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Chama alisema kuwa malengo yake ni kuona timu inapata matokeo na wala sio jambo lingine lolote hivyo kuwa timu imepata matokeo kwake ndio furaha zaidi.

“Ni fuaraha kuona timu imepata matokeo na hilo ndio la msingi zaidi na ndio kipaumbele kwa kila mtu ambaye yupo hapa Simba, sio wachezaji kocha wala viongozi na hata mashabiki

“Wote lengo letu ni moja yaani kuhakikisha na kuona timu inashinda hivyo nimefurahi tumepata matokeo mazuri na hayo mengine ambayo yamejitokeza wala sio yamuhimu sana,” alisema kiungo huyo. Msimu huu kwenye ligi amecheza mechi 17 ambapo amefanikiwa kufunga mabao matatu na kutoa asisti 12.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Tanzania Zipo HAPA

Ufadhili wa Masomo ( Scholaships) Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments