Dawasa Wafunguka Mtambo wa Maji Ruvu Chini Kuzimwa Kuanzia Kesho

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imewatangazia Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini uliopo Bagamoyo, kuwa mtambo utazimwa kwa saa 36 siku ya Jumatatu January 30,2023.

“Lengo ni kuruhusu kufanyika kazi ya kusafisha mifumo yote ya mtambo ikiwemo machujio, matanki yote ya maji na mabomba makuu yote ya kusafirisha maji kutoka katika mtambo huo, kutokana na kazi hiyo, maeneo yanayohudumiwa na mtambo huo yatakosa huduma ya maji kuanzia Jumatatu asubuhi hadi Jumanne jioni”

“Maeneo hayo ni Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Zinga, Kerege, Mabwepande, Bunju, Kunduchi, Mbezi Beach, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaki, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Uwanja wa ndege, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya mji”

“Mamlaka inawaomba Wananchi kukumbuka kuhifadhi maji ya kutosha ili kuweza kuyatumia kipindi chote cha matengenezo, DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad