Marcus Rashford Awajibu Kwa Vitendo Mashabiki Kwa Sasa Ndiye Shujaa Man United

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MWANZONI mwa msimu huu, Marcus Rashford hakuwa kwenye kiwango kizuri, huku akifanikiwa kucheza mechi sita mfululuzo na kufunga mabao matatu, kabla ya kuumia na kumtibulia zaidi.

Nyota huyo wa Manchester United, kwa sasa ndiye shujaa wao kutokana na kufunga mabao muhimu ya kuamua matokeo kwenye michuano yote.

Rashford ambaye katika michuano ya Kombe la Dunia 2022 alifunga mabao matatu, tangu kumalizika kwa michuano hiyo, kila anaposhuka dimbani akiwa na klabu yake ya Manchester United, anaweka mpira nyavuni.

Nyota huyo kwa sasa ameonekana kuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa timu pinzani kutokana na kufunga mfululizo hadi anawakera wapinzani.

Tayari kwenye Premier amefunga mabao saba msimu huu akicheza mechi 17, kuna uwezekano mkubwa akafunga mabao mengi zaidi kuliko misimu mingine yote kikosini hapo tangu 2015/16.

Rekodi zinaonesha kwamba, Rashford msimu ambao alifunga mabao mengi Premier ni 2019/20 akifikisha 17 katika mechi 31, hivyo ana deni la mabao kumi kuifikia rekodi hiyo, huku timu yake ikisaliwa na mechi 21.

Ukiangalia msimu wa 2017/18, Rashford alifunga mabao 7 Premier baada ya mechi 35, hivyo msimu huu tayari ameifikia rekodi hiyo kwa mechi chache zaidi.

Kwa sasa kilichobaki kwake kwenye mechi 21 zilizosalia, anahitaji kuivunja rekodi ya msimu wa 2018/19 alipofunga mabao 10 kwenye mechi 33 na 2020/21 wakati akifunga mabao 11 kwa mechi 37, kabla ya kuifikia ile ya msimu wa 2019/20.

Msimu mbaya zaidi kwake ulikuwa ule uliopita 2021/22 alipofunga mabao 4 kwenye mechi 25 za Premier, kipindi hicho aliandamwa sana na majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Rashford tangu kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia 2022, ameitumikia Man United kwenye mechi 5 na kufunga mabao 5. Amefunga kila mechi, huku akitoa asisti 3, hivyo amehusika kwenye mabao 8.

Katika michuano yote msimu huu upande wa klabu, Rashford amefunga jumla ya mabao 13, asisti 6, kwenye mechi 24.

Anachokifanya Rashford hivi sasa ni kama anajibu kwa vitendo kile ambacho wengi walikuwa wakisema kwamba ameshuka uwezo na hataweza kuisaidia timu hiyo.

Kumbuka wakati Man United inaachana na Cristiano Ronaldo, Rashford ndiye alikuwa mtu wa kwanza zaidi kuangaliwa ataisaidiaje safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kabla hajaletwa straika mpya.

Lakini katika mechi hizo tano zilizopita, ni wazi straika huyo amejibu kwa vitendo kwamba anaiweza kazi hiyo endapo tu akiwa fiti. Hapa Man United wote kwa ujumla wanaomba Rashford asikumbwe tena na majeraha kama awali.

Licha ya hivyo, lakini bado Man United chini ya Kocha Erik ten Hag, inatakiwa kufanya usajili wa straika mwingine kuongeza nguvu eneo hilo ili iwe salama zaidi kwao katika mbio za kufikia malengo yao msimu huu ya kumaliza ndani ya nne bora kwenye msimamo wa Premier.

STORI: OMARY MDOSE

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad