Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza kuondoa utaratibu wa kutangaza Shule 10 bora na Watahiniwa 10 bora kwa matokeo ya mitihani mbalimbali kwakuwa utaratibu huo hauna tija.
Akiongea Dar es salaam leo wakati wa kutangaza matokeo Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athuman Amas, amesema “Tumeondoa utaratibu wa kutangaza Shule 10 bora au Watahiniwa 10 bora kwasababu hauna tija, tunawafananisha Watu ambao wamefanya mtihani sawa lakini mazingira tofauti”
“Tulizoea kusikia lugha za Top 10 sijui ‘Wasichana wawagaragaza Wanaume’, tuondokane na mazoea, ukigundua jambo unalolifanya halina tija hauna haja ya kuendelea nalo, unamtaja Mtu ameongoza na kumlinganisha na Watu ambao hawakusoma katika mazingira yaliyofanana sio sahihi”
“Kama kuna Shule ulikuwa unasubiri itangazwe kuwa kwenye Top 10 hiyo haipo, kwanza kutangaza Shule ya kwanza huenda tulikuwa tunakufanyia marketing (kukutangaza kibiashara), tumeona haina tija”
0 Comments