Ticker

6/recent/ticker-posts

Serikali : Wanafunzi Shule za Umma Ruksa Kuvaa Suruali Kisa Baridi Kali

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


WAZAZI na walezi jijini Mbeya, wamepokea kwa mikono miwili, maamuzi yaliyotolewa na serikali, kwamba wanafunzi wa shule za umma, wasichana na wavulana waanze kuvaa suruali, kutokana na mazingira ya Mkoa huo uliopo nyanda za juu Kusini, kuwa na baridi kali.

Kamishna wa Elimu nchini, Dk. Lyabwene Mtahabwa.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wazazi na walezi jijini humo, baada ya kikao kati ya wazazi, walezi katika shule msingi Mapinduzi, kwamba serikalikupitia vikao maalumu, waidhinishe aina ya sare, kulingana mazingira yao.

Mfumo wa shule za umma zilizo nyingi nchini, wasichana huvalia sketi za bluu na wavulana kaptura na wote shati nyeupe, lakini sasa ruhksa kuvaa suruali kutokana na hali ya hewa.

Martha Mwakilamo, mkazi wa jijini humo anasema: " Ni heri watoto wavae suruali hasa hawa wadogo, Mbeya ni baridi sana, hivyo hapo awali mwanangu alivaa kaptura na ilinibidi nimvalishe soski hata jozi tatu ili apate joto miguuni."

Kamishna wa Elimu nchini, Dk. Lyabwene Mtahabwa akizungumza na Nipashe kwa njia simu, hivi karibuni, amethibitisha hilo na kwamba mikoa, Wilaya kupitia vikao maalumu na kushirikisha jamii, wapange sare za kuvaa wanafunzi kulingana na mazingira.

"Mwongozo ulitoka, sare wanafunzi wa shule za umma inalingana na mazingira, waamue zivaliwe za mfumo gani, ila isitofautiane rangi," kamishna huyo ameiambia Nipashe.

Julai, mwaka jana, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ilisema kwamba hali ya baridi katika mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya baridi ilifikia viwango vya chini vya nyuzi joto 4°C.

By Christina Mwakangale

Post a Comment

0 Comments