Aliyepewa dhamana kesi ya wizi, auawa akiiba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Dar es Saalam. Mkazi wa Mtaa wa Ihira, Kata ya Buhongwa mkoani Mwanza, David Deogratus (32) ameuawa na wananchi wenye silaha za jadi baada ya kumshambulia akidaiwa kuiba runinga nyumbani kwa mwalimu wa Shule ya Msingi Kilumba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP  Mutafungwa alisema hayo Jumamosi 25, 2023 na kufafanua kwamba hata hivyo mtuhumiwa huyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu.

Amesema mtuhumiwa huyo inadaiwa baada ya kuiba runinga (flat screen) aliruka dirishani ndipo wananchi walipomuona na kumvamia. Pia miongoni mwa vifaa alivyokutwa navyo ilikuwa ni nyundo, bisibisi na spana ambavyo inaelezwa alivitumia kwenye shughuli zake za kihalifu.

Askari waliokuwa doria walifika eneo la tukio kisha kumnusuru na kumuwahisha Hospitali ya Bugando kwa ajili ya matibabu.


Kamanda ACP Mutafungwa amesema baada ya kupitia kumbukumbu zake za kiuhalifu, wamebaini kwamba alitoka Gereza la Butimba  Machi 22, mwaka huu.

“Alitoka kwa dhamana na awali alikuwa akishtakiwa kwa kosa la wizi ambalo kesi yake ya jinai  ndiyo ilikuwa imemuweka hapo gerezani,” amefafanua.

Kamanda Mutafungwa amesema mtuhumiwa huyo enzi za uhali wake alitoka gerezani Machi 22, 2023 na kukaa uraiani siku moja, kisha kuangukia kwenye tukio jingine la wizi lililoababisha kupigwa na wananchi.


“Niwatahadharishwe wahalifu wanaopata dhamana, kama mtu ametuhumiwa na kosa la kijinai, anapokuwa nje anatakiwa kuendelea kuwa raia mwema. Asijihusishe kabisa na vitendo vya kihalifu. Hata hivyo Jeshi la Polisi tunawatafuta watu waliofanya tukio hilo la kujichukulia sheria mkononi,” amesisitiza.

Jeshi hilo limetoa onyo kwa wananchi wote wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake wanapopata taarifa watoe taarifa kwa jeshi hilo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad