Ally Mayay Aula Jumuiya Madola

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), anawajulisha wadau wa michezo na Watanzania wote kuwa Taifa letu limeteuliwa kuwa Mjumbe katika Bodi ya Ushauri wa Michezo ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth Advisory Body on Sport –kwa kipindi cha miaka mitatu
Hatua hiyo inatokana na kuimarika kwa nchi yetu katika nyanja za diplomasia ikiwemo ya michezo katika uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa uteuzi huo, Bw. Alli Mayai Tembele ataiwakilisha Tanzania katika Bodi ya CABOS na kuwa Mjumbe mwakilishi wa Bara la Afrika. Bw. Alli Mayay kwa sasa ndiye Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo nchini. Kiuzoefu Bw. Alli Mayay ni mwanamichezo nguli na Nahodha mstaafu wa Timu ya Taifa ya (Taifa Stars) na ni kocha wa mpira wa miguu kitaaluma.

CABOS ni chombo cha kumshauri Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na Serikali wanachama kuhakikisha kunakuwepo ushirikishwaji thabiti wa Serikali na uwakilishi katika maendeleo ya sera na utekelezaji wake kwa kuzingatia maadili na matarajio yaliyowekwa ndani ya Mkataba wa Jumuiya hiyo.

Waziri Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), anampongeza Bw. Mayay na kumtakia uekelezaji mwema wa majukumu yake.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad