Baada ya Mo Dewj kusema amemsamehe Haji Manara,mwenyewe aibuka asema haya,awachana hawa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Haji Manara Ameandia Haya: 

Huko nyuma nilipojiunga na Champions, hawa wafanya interview za kujitafutia Rizki ya kula, waliandika hilo ndio anguko la Haji, haikuwa kwa Uwezo wa Allah..


nilipofungiwa waliandaa hadi Party Kwamba nimekwisha, Mungu yule yule akakataa,


Brand iliyojengwa kisawa sawa haifi kwa maneno ya Wagagagigikoko ila ni Kwa kudra ya Mungu tu , bado nna endorsements za nguvu kuwazidi,bado natajika kila eneo, mmebakia uchawi na uchawi tu.


Sasa wanahangaika na kunisingizia uongo mpya, hivi mimi ni nani nimtukane Mtu kisha Mamlaka za Nchi ziniache? Unamuuliza swali Source eti Huku nyuma Haji alikuwa anakutukana sana mitandaoni, je akikuomba radhi utamsamehe? Mohamed aone nimemtukana aniache?


Mwandishi hopeless kabisa.


Leading question lenye upumbav wa juu, nia hapo ni kuonyesha taswira mbaya dhidi yangu, Good luck mimi sina ugomvi na Mohammed, tumetofautiana kikazi,Yeshaaaaa!!


Pls Waandishi wenzangu, mnapokwenda kufanya mahojiano na Watu, Muulize maswali ya maana sio kuuliza maswali ya kufurahisha Tumbo ili kesho libehue.Tunazo changamoto nyingi za kupata majawabu, Haji mumuache tu, ni kitu kingine kabisa, kutwa Haji Haji.


Sijawahi kumtusi Mohamed na kama lipo liwekwe hadharani hilo tusi, labda kusema Bilioni ishirini hazijawekwa benki ndio tusi .na infact simlaumu kabisa Mudi, amefosiwa ajibu vile kwa maslahi yao, huyu ni Tajiri ningemtusi mida hii nipo na Sabaya mahali.


Naombeni niachieni mimi ni mfungwa ,mnahangaikaje na mtu aliyefungiwa?


Mimi kitambo kirefu nimetulia huku Kwa Wananchi wenzangu, shida ya nini sasa, mnapambana na kivuli changu Mchana hadi Usiku, mnaumia na matakwa ya Allah?


Nb: kadri mnavyonijadili hiki kipindi nikiwa nje ya football mnanisaidia kuniwekea brand yangu juu, nzuri mno hii kwangu🙏🏻🙏🏻 Msiache, Ndegelec

Mr Mohammed.

Kwa mila za kwetu na kwa Utamaduni wa kidarisalama ,Mji niliozaliwa na kukulia, na Kwa kuzingatia Sheria na kanuni za Mamlaka yetu ya kinchi, lakini kubwa zaidi, kwa Misingi ya Imani yetu, inanipasa niseme Sorry pale nilipokosea, but ni vema mkaja tena huku mitandaoni kuyaanika hayo matusi niliyowahi kuwatusi ili niwaambie Samahani, otherwise ni uchale, kiki na kutaka kuchafua Watu tu.


Inawezekana vipi Mwanadamu unaejinasibu ni Tajiri namba moja Afrika kupost mara kadhaa tena mfufululizo, ukimsingizia Muomba Mungu bila kuweka ushahidi? why iwe leo? Kwa nini msinishtaki? Nilikutusi Inbox au katika cm?


Unaweza kuajiri Mawakili wa dunia nzima, unaweza kutumia utajiri wako kunifunga milele Gerezani, Why unakubali kusamehe mahali ulipoona umekosewa? Tena hujawahi kuombwa msamaha? Hv mm na ww kaka nani anaestahili kumuomba msamaha mwenzie?


Sitasahau nilipodhulumiwa kwa kuwekwa ndani Kwa ajili yako, bado ulipopatikana hata Sorry ulishindwa kuniambia, huku ukijua Sijui lolote kuhusu kutekwa kwako.


Ila always nilikupa heshma kubwa kama kiongozi wangu lakini uliwahi hadi kuja hadharani kuwakataza Wachezaji wako wasinipost na ukatambia utajiri wako kwamba ww ndio unawalipa, Shekh mm ni Mtoto wa kimaskini lakini nimeridika na majaaliwa yangu, usinichafue ili upate utukufu, why hamnishtaki kama niliwatukana?


Mnatengeneza Cinema upya ilioisha miaka kadhaa nyuma kisha hamweki ushahidi? Serikali ya Tanzania hii hii inayozingatia Utu wa Mtu iniachie nikutusi, kisha nisichukuliwe hatua ?


Kaka yangu nakujua vizuri , umetafuta attention ya kuzungumziwa tu,ila usinilazimishe niseme niliyosamehe, Pls Pls Tajiri wa kwanza Afrika.


Nimefungiwa lakini bado kutwa ni Haji, Basi hata wewe Boss? Kwani without Haji hakuna Story? Trend ni mimi tu.


Waomba Mungu wenzangu naweza kuwaelewa ni Njaa tu, ila sijawahi kufikiria hata ww Shekh, Usiku wote unapost kuhusu mm tu, halaf why hutag jina hili kubwa?


Ok my former Boss, tambua kitu kimoja tu, I have nothing to loose nikiamua na mimi niseme,,Chonde Chonde Chief, Principle yetu kuu huku uswazi, kuzaliwa na kufa ni ahadi ya Maulana.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad