Kumekucha...Kumbe sio Mavokali Msanii Mpya WCB, Mkubwa Fella Atoa Siri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kama ulikuwa unadhani msanii mpya aliyesainishwa hivi karibuni na label ya WCB kuwa ni Mavokali hilo toa akilini mwako, Fella amekanusha sio msanii huyo waliyemsainisha.


@mkubwafellatmk ambaye pia ni mmoja wa mameneja wa WCB amesema, "Kwanza sio yeye, halafu msanii (aliyesainishwa) anatoka Temeke ila simtaji, itakapofika wakati Nasib (Diamond) mwenyewe atamtaja" - Ameeleza Fella akiiambia Dizzim Online kwenye mahojiano yake mapya.


Itakumbukwa, mwimbaji wa kizazi kipya na hitmaker wa "Mapopo" msanii @mavokali_ aliingia kwenye headlines mnamo February 2 baada ya mchana wa siku hiyo, Boss wa lebo ya WCB, msanii @diamondplatnumz kuweka wazi ameingia mkataba na msanii mpya ambapo ali-share sehemu fupi ya picha katika mkataba huo na kuambatanisha ujumbe huu, "02/02/2023 Another Blessing day for the blessing kid".


Aidha, @diamondplatnumz hakuweka wazi juu ya jina wala jinsia ya msanii huyo mpya na hata kuhusu lini atatangazwa rasmi, sasa saa chache baadae (siku hiyo hiyo) Mavokali kupitia insta story yake akaandika "02/02/2023 Deal Done" akiwa na maana tarehe 2 mwezi wa pili kuna dili amelikamilisha.


Hivyo, mashabiki na wadau mbalimbali wakawa wanauhusisha ujumbe huo wa @mavokali_ na taarifa mpya ya Diamond kuwa ndio ingizo jipya katika lebo hiyo ambayo hadi sasa ina jumla ya wasanii watano pekee.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad