Leonora: Nilicheza 'Bushman' nikiwa na miaka 5, sijalipwa mpaka leo miaka 42

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Muigizaji wa Namibia, Leonora Jacobs aliyeigiza kwenye filamu ya “The Gods Must Be Crazy” ya mwaka 1989 anasema hajawahi kulipwa kwa kazi aliyoifanya katika filamu hiyo.


Sasa hivi ana umri wa miaka 42 na anaishi nyumbani kwao na mama yake akiwa na maisha duni wakati filamu aliyoigiza ambayo Kibongobongo filamu hiyo inafahamika kama 'Bushman' ilimpa umaarufu na ilitengeneza Tsh bilioni 15.


Leonora alikuwa ana umri wa miaka mitano wakati filamu hiyo inaandaliwa mwaka 1985, na alipewa ahadi atalipwa pesa zake akifikisha miaka 21.


“Mimi ni mmoja kati ya waigizaji waliocheza filamu ya ‘God Must Be Crazy’ sehemu ya pili, ilikuwa mwaka 1985 nikiwa na umri wa miaka mitano tu na sasa nina umri wa miaka 42. Sehemu niliyocheza mimi ni ile ambayo nilicheza na fisi.


“Ninadhani nilitakiwa kupata chochote kutokana na ile kazi niliyoifanya kwenye uhusika wangu, lakini mpaka leo sijawahi kupata chochote. Walituahidi nikifikisha umri wa miaka 21 watanilipa lakini mpaka leo hakuna chochote," amesema Leonora.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad