Mambo ya Kuzingatia Unapokuwa Mgeni Nyumbani Kwa Watu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




1. NJOO NA MAHITAJI YAKO MADOGODOGO
Njoo na mswaki wako, sabuni yako ya kuogea na dawa yako ya mswaki, taulo na mahitaji yako mengine madogomadogo. Kuna wageni wanaomba hadi nguo za...kwa wenyeji sio vizuri.

2. USIFUNGUE FRIJI WALA MAKABATI
Usifungue friji ya wenyeji au makabati bila kuambiwa ufanye hivyo. Mgeni unasikia kiu omba maji kwa wenyeji sio unaanza kufungua friji bila ruhusa eti unatafuta maji ya kunywa. Ukihitaji kitu omba kwa wenyeji sio kuanza kupekuapekua.

3. USIBAKI SEBULENI
Wenyeji wakiingia kulala usibaki sebuleni unatazama TV ingia chumbani kwako. Sambamba na hilo mkiwa mnatazama TV sebuleni usianze kushika rimoti na kubadili channel bila ruhusa ya wenyeji.

4. USIZIDISHE MUDA WA KUKAA
Ukifika ni vizuri uwajulishe wenyeji wako utakaa hadi lini na usizidishe muda labda wenyeji wakuombe wenyewe. Kama uliwaambia utakaa wiki ikifika ondoka sio unasubiri hadi wakuulize unaondoka lini.

5. USIINGILIE MAZUNGUMZO
Ikatokea wenyeji hasa mke na mume wana mjadala wao wa mambo yao binafsi usipende kuingilia na kujifanya mshauri bila kuombwa kufanya hivyo. Labda wanapanga wapike nini siku hiyo mgeni usharukia kuchagua chakula kaa kwa kutulia. Katika jambo lolote wanalojaldili subiri uombwe ushauri.

6. USITEMBELEE MAJIRANI
Usitembelee majirani "ooh jamani mie ndo mpwa wa huyu jirani yenu nimeona niwasalimie".... Pata ruhusa ya wenyeji wako kwanza kabla hujaanza kuzunguka kwa majirani. Sambamba na hilo usilete wageni hapo ulipofikia bila kumtaarifu Mwenyeji wako.

7. KULA VYAKULA VILIVYOPO
Jitahidi kula chakula kinachowekwa mbele yako na kama vinakupa shida basi nunua hivyo vyakula sio "ooh maharage yananiumiza tumbo" kanunue nyama ulete wakupikie.

8. USITUMIE VIFAA VYA WENYEJI
Usianze kutumia vifaa vya wenyeji bila ruhusa mfano unaanza kuwasha computer au vifaa vya mazoezi . Usianze kuzunguka nyumba na kuingia kila mahali labda mwenyeji wako akuoneshe sio kukagua nyumba nzima na kuingia vyumba ambavyo hujaambiwa.

9. SAIDIA KAZI
Tandika kitanda chako na safisha chumba ulichopewa kulala. Saidia kazi za hapo nyumbani ulipofikia labda wakukataze wenyeji. Sambamba na hilo utakapoondoka acha chumba katika hali ya usafi kama ulivyokikuta.

10. USIJE MIKONO MITUPU
Usije mikono mitupu beba zawadi kidogo kwa wenyeji wako.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad