Mfalme Zumaridi "Sajuki ninaye Yupo Hai, Wastara tulia Nitamfufua"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mhubiri maarufu jijini Mwanza asiyeishiwa vituko, Diana Bundala maarufu kama "Mfalme Zumaridi" amesema kuwa aliyekuwa mwigizaji maarufu wa Bongo Movies, Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki aliyefariki Dunia Julai 2, 2013 yupo hai.


Zumaridi amesema hayo kufuatia aliyekuwa mke wa Sajuki, mwigizaji Wastara Juma kumvaa na kumtaka aache kuwaumiza watu kwa kudai kuwa atawafufua waliokufa kama Kanumba na Sajuki ambao anadai kuwa anaishi nao na anazungumza nao kila siku.


"Nilishawahi kusema nilichukuliwa na Mungu kwa umbo la Simba nikapelekwa kuzimu nikiwa darasa la tatu, nikaonyeshwa amisukule, mpaka leo ninaishi nao.


"Wastara naye nasikia amenitukana, sasa nataka nimwambie kwamba mume wake Sajuki yupo, yupo, yupo hai, hata hapa napoongea yupo anasikia.


"Nikiongea watu wanaweza kusema Zumaridi ametoka gerezani amekuwa mwehu au chizi ama taila lakini ndivyo ilivyo," amesema Zumaridi ambaye hivi karibuni ametoka gerezani baada ya kumaliza kifungo chake cha mwaka mmoja.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad