Ticker

6/recent/ticker-posts

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Atoa Ufafanuzi Toto Afya Kadi

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), imesema watoto ambao awali walikuwa wakisajiliwa kupitia utaratibu wa bima ya afya ya ‘Toto Afya Kadi,' sasa watasajiliwa kupitia vifurushi vya bima ya afya au shule wanazosoma ili kufanya maboresho zaidi ikiwemo malalamiko yanatolewa na wananchi.

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga amesema wakati wa maboresho hayo watoto waliolipia kadi zao wataendelea kupata matibabu lakini kwa wale ambao wanataka kujiandikisha watasajiliwa kupitia shule zao.

“Tunashukuru mpaka sasa tuna shule nyingi tu ambazo zimeonesha nia na wengine kwao ni fursa kuvutia watoto shuleni wameshaanza kuja maofini kwetu na kutafuta namna bora ya kushirikiana na hizo shule ili sasa waweze kuingiza Watoto kwa umoja wao,” amesema

Konga amesema faida moja wapo ya kusajili mashuleni ni dhana ya bima ya afya kujengeka mapema kwa watoto, matarajio ya kusajili watoto wengi yatafikiwa lakini pia wakati maboresho yanafanywa kwenye eneo la usajili na huduma watoto wanaotaka kuingia hawatoweza kukosa huduma zinazotarajiwa.

Post a Comment

0 Comments