Baba wa Martha Afunguka Tena "Martha Alikuwa na STRESS Sana, Alinigusia Anachopitia"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mzee Ndeonasia Towo ambaye ni Baba Mzazi wa Neema Towo au kwa jina jingine Martha (30), Mfanyakazi wa BOA BANK Tawi la Kahama, Shinyanga ambaye ameuawa na Watu wasiojulikana kwa kummwagiwa Petroli na kisha kumchoma moto na kumsababishia kifo, amesema Mtoto wake kabla ya kuuawa alikuwa na stress na kulazimika kutoka Kahama na kurudi kwa Wazazi wake Kibaha ili kuongea nao na alishawaambia machache kati ya mengi yaliyomsababishia stress.


Kwenye mahojiano yake na Mtangazaji na Mwandishi wa Habari Bakari Chijumba wa @ayotv_, Mzee Towo ambaye ni Mkazi wa Kwa Mbonde, Kata ya Kwa Mathias, Wilaya ya Kibaha amesimulia kilichomtokea Martha siku ya tukio huku akisema kwa sasa hatoeleza kwa kina aliyoambiwa na Mtoto wake ili kuepusha kuingilia uchunguzi wa Polisi na Vyombo vingine vya usalama.


“Martha alikuwa na stress, alikuwa stressed, she was stressed, kwahiyo alirudi Kibaha ili kutuelezea Wazazi wake yanayomsibu na ametueleza machache, angenieleza yote labda ningejua zaidi lakini three.. three….quarters of the information i have but nataka Jeshi la Polisi lifanye kazi yake”


Mzee Towo amesema anaamini kifo cha Mwanae hakijachangiwa na la wivu wa kimapenzi bali vitu vingine “Martha hakuwa Mtu wa ugomvi na kamwe sijawahi kusikia amegombana na Mtu na hakuwa na Boyfriend Kibaha, alikuwa anajiandaa kuolewa mwaka huu ana Boyfriend wake, Mchumba alishamleta nyumbani”


“Mchumba wa Martha alikuja tangu tukio lilivyotokea amekaa na sisi mpaka msiba umetokea, Wazazi wake wote kuna Watu kama 8 wa kutoka Mbeya wamekuja, Boyfriend wa Martha ni Mtu wa Mbeya na alikuwa anafanya kazi Arusha, walikuwa hawaishi pamoja na Martha”

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad