Mtia nia Urais TLS Kukata Rufaa Baada ya jina Lake Kuenguliwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Mtia nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili, Tanganyika ( TLS), Sweetbert Nkuba, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 23,2023 juu ya uamuzi wake w kukata rufaa kupinga ya jina lake kuenguliwa katika kinyang'anyiro hicho.

Dkt. Aloys Rugazia wakili wa Sweetbert Nkuba akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Machi 23, 2023 juu ya uamuzi  wa mteja kukata rufaa kupinga jina  lake kuenguliwa katika kinyang'anyiro hicho cha kugombea kiti cha Urais TLS

MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Sweetbert Nkuba amelaani kuenguliwa kwa jina lake kwenye hatua za awali za mchakato wa uchaguzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Machi 23, 2023, Nkuba amesema anatarajia kukata rufaa kupinga uamuzi huo uliotangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TLS, Charles Rwechungura hivi karibuni.

Nkuba amesema kuwa anazo sifa za kuwa mgombea na kwamba ameshangazwa na kitendo cha kuenguliwa kwa jina lake kwa hoja ya kuwa aliwahi kuwa mtumishi wa serikali pia hakuwahi kuhudumu shughuli za uwakili kwa muda wa miaka kumi.

"kwa mujibu wa sheria yetu na kanuni za uchaguzi za TLS nina sifa za kugombea ...kulikuwa na hoja mbili hoja ya kwanza sikuwahi kufanya kazi ya uwakili kwa miaka kumi pili niliwahi kuwa mtumishi wa serikali sababu hizo sijakubaliana nazo kwani tangu nimeapishwa kuwa wakili huu ni mwaka wa 13 au 14 ni zaidi ya miaka 10 pili ni kweli nilikuwa mtumishi wa serikali na nilishaacha kazi serikalini kwa kufuata taratibu zote za kisheria kwa hiyo kamati imetumia maneno ya fununu kutoa uamuzi lakini sitaki kueleza sababu kiundani kwa kuwa nina jopo la mawakili walionipendekeza kuwania urais wakiongozwa na Jeremiah Mtobesya hivyo jopo linafanya utaratibu wa kukata rufaa" alisema Nkuba.

Nkuba amesema kuwa anataka kukata rufaa ili haki ionekane imetendeka lakini pia kuhakikisha uwepo wa demokrasia kwenye vyama vyote vya kitaaluma ili kitendo hicho kisijitokeze tena.

Naye Dkt. Aloys Rugazia Wakili wa Nkuba ambaye atamwakilisha mbele ya kamati ya Rufaa ya TLS amesema kuwa kigezo kilichotumika kumng'oa mteja wake ni cha kibaguzi kwakua kufanya kazi serikalini haiwezi ikamtia Wakili dosari kiasi hicho.

"Mteja wangu alinipigia simu nikapitia uamuzi uliotolewa na kamati na nimeona kuwa kuna mambo yanahitaji ufafanuzi kwa sababu yanaibua utata kwa mfano wanasema mteja wangu alikuwa mtumishi wa serikali kwa hiyo kwa mujibu wa taarifa za TLS mteja wangu amefanya kazi ya uwakili miaka miwili wanajaribu kutoa kile kipindi alichotumikia serikali mimi naona ni ubaguzi kwa watu waliotumikia serikali" alisema Rugazia.

Dkt. Rugazia amesema kuwa watafika mbele ya kamati ya Rufaa ya TLS ili kupata tafsiri ya kufanya kazi ya uwakili kwa kipindi cha miaka kumi kuna hesabiwa kwa kigezo kipi.

"Nafikiri tafsiri ya kufanya kazi ya uwakili iangaliwe ni lini aliapishwa na kukabidhiwa cheti cha uwakili nafikiri ni uamuzi unaotakiwa utazamwe upya" alisema Dk. Rugazia.

Dkt Rugazia amesema kuwa rufaa yao ikigonga mwamba mbele ya kamati basi watalazimika kutoka nje kwenda Mahakama Kuu kukata rufaa. Aidha Rugazia ameeleza kuwa wanayo imani kuwa kamati ya Rufaa ya TLS ikiongozwa vyema itatoa maamuzi ya haki!

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad