PEP Guardiola Aitaja Arsenal Kuwa Timu Bora Premier League Msimu Huu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

PEP Guardiola

PEP Guardiola ameitaja Arsenal kama timu bora msimu huu ndani ya Premier League, ikiwa inaikimbiza Manchester City katika kuwania ubingwa.

Arsenal wapo juu ya msimamo wa Premier, wakiifunika Man City iliyo nafasi ya pili ambapo kabla ya mechi za jana, tofauti yao ilikuwa ni pointi tano.

Msimu huu, Arsenal wanapambana kusaka taji hilo ambalo mara ya mwisho walilibeba 2003/04, huku msimu wa 2015/16 wakimaliza nafasi ya pili.

Bosi huyo wa Man City, amesema anafikiria kuwa Arsenal ndiyo timu bora ndani ya ligi hiyo msimu huu.

“Kwa sasa wao wamekuwa tishio, wamekuwa na mabadiliko, kwenye mipira ya kutengwa wako vizuri, ndiyo maana kwangu naona wao ni timu bora.

“Hawajakuwa nafasi za juu (top four) kwa muda mrefu na ilikuwa kama wanahitaji muda, lakini kwa sasa wako vizuri, msimu huu wamejipanga.

“Kile ambacho wanakifanya Arsenal kwa sasa kila mmoja anakiona, hakuna siri,” alisema Guardiola.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad