MASKINI: Mtoto wa Marehemu Ruge, Aomba Nandy Kumpa Kazi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mtoto wa aliyekuwa mrasimu na mkurugenzi wa mikakati na maendeleo katika kampuni ya Cloud Media, Ruge Mutahaba, Mwachi Mutahaba amejitokeza akisema kwamba anapitia maisha magumu sana maishani mwake licha ya babake kuwa jina kubwa kwenye tasnia ya habari na Sanaa.

Mwachi ambaye huonekana kwa nadra mno hadharani safari hii alionekana katika runinga ya Wasafi ambapo alishiriki mahojiano ya kipekee na kufunguka ukweli mzima wa maisha tangu kifo cha baba yake mwaka 2019.


Itakumbukwa vizuri kwamba jina la Ruge Mutahaba katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, ni jina kubwa sana kwani inasemekana kwamba asilimia kubwa ya wasanii ambao wanatamba mpaka sasa nchini humo walipitia mikononi mwa mrasimu huyo.

Kipindi cha uhai wake, Ruge alichakarika mno mpaka kukikuza kipaji cha Nandy, mmoja wa wasanii wa kike wanaofanya vizuri mno katika Sanaa ya muziki wa kizazi kipya.

Miaka mitano mbele baada ya kifo chake, mtoto wake mkubwa Mwachi amejitokeza akidai kwamba anapitia maisha magumu sana, na kutoa wito kwa Nandy kurudisha jicho nyuma na kulipa fadhila za marehemu Ruge kwa familia yake.


Mwachi alifunguka kwamba kipindi cha nyuma alikuwa DJ wa Nandy lakini baada ya kuzongwa na mambo mengi ikiwemo kusimamia urithi wa baba yake, ilibidi ameiachia ile nafasi kwa mtu mwingine, lakini safari hii anarudi akimtaka Nandy kumpa kazi yoyote.

“Ile nafasi ya DJ wa Nandy watu wengi walikuwa wanaing’ang’ania na wakati huo mimi mwenyewe nilikuwa na urithi wa babangu kufuatilia. Nikasema hiyo nafasi sina haja kuwanyima watu. Nikaippatiana kwa DJ mdogo huko Bukoba, sasa sijui hapo ilikuwaje. Lakini kama Nandy ako sawa mimi kurudi sasa hivi mimi nipo radhi maana vitu vimenitoka,” Mwachi alisema.

“Ikiwezekana na kama anaangalia, ninaomba kazi kwake!” Mwachi aliongeza.

Mwachi alisema kwamba watu wengi huwa wanamuona akiwa katika maisha ya kawaida na kuanza kumkejeli, wakidhania kuwa mtoto wa mtu mkubwa kama Mutahaba, hafai kuwa katika maisha hayo.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad