Aliyejirusha Ghorofani na Kufariki Makumbusho Atambulika, ni MC Maarufu Joel

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema linachunguza tukio la kifo cha Mtu aitwae Joel Misesemo Chizi anayekadiriwa kuwa miaka kati ya 35 hadi 40, Mkazi wa Mwananyamala ambaye alijirusha kutoka ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho Kijitonyama na kufariki.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Marehemu alionekana katika jengo hilo leo tarehe 23, Mei 2023 majira ya saa kumi na moja alifajiri na alimwambia Mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye Msikiti uliopo ghorofa ya 15 dani ya jengo hilo lakini muda mfupi baadaye alijirusha.

Taarifa ya Polisi imesema camera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani na kufariki ambapo tayari mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.

Jeshi la Polisi limepata gari la Marehemu aina ya Suzuki rangi ya silver lenye namba za usajili T142 DRM lililokuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya magari katika eneo hilo na sasa limehifadhiwa Kituo cha Polisi Oysterbay.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad