Mgunda ampa ujumbe mzito Ally Kamwe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kocha msaidizi wa Simba, Juma Mgunda ametoa kauli nzito kwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe ambaye hivi karibuni alimtolea maneno ya kejeli kwenye hadhara.

Mgunda ameiambia Mwanaspoti kwamba hata kabla ya Kamwe kumuomba msamaha, yeye alishamsamehe kwa kauli isiyokuwa ya staa aliyoitoa dhidi yake.

"Sijaonana naye ana kwa ana, lakini amenipigia simu usiku na kuniomba msamaha, lakini hata kabla hajakumbuka kufanya hivyo mimi tayari nilikwisha msamehe," amesema Mgunda na kuongeza;

"Hata hivyo katika maisha anapaswa kukumbuka kitu kikubwa ni heshima bila kujali cheo cha mtu, ufadhili wake kwako au kumuangalia sura yake, kwani ukitoa kashfa kwa kudhamiria inakujengea mazoea na kesho au keshokutwa utamkosea mwingine na mwingine huenda akafika hadi kwa yule anayekufadhili," amesema Mgunda


Amesema kashfa za Kamwe dhidi yake ziliwakwaza wengi na alipaswa kuwaomba radhi na wengine wote walioguswa na jambo hilo na si kumuomba yeye Mgunda pekee, japo yeye alikwishamsamehe hata kabla hajafanya uamuzi wa kuomba radhi ila kuna wengi wanaomzunguka wamekwazika pia.

"Mimi ni muumini wa dini ya Kiislamu, katika maisha tunaambiwa tusamehe 7 mara 70 na tayari nimefanya hivyo, ingawa kwa umri wa Kamwe anapaswa kulichukulia hili kama funzo, tujifunze kuchunga midomo yetu.

"Kamwe ni mwanangu tena mdogo ninao wakubwa kuliko yeye, alipopima na kuona kuna uzito kuomba msamaha mimi sina shida, moyo wangu kwake ni mweupe ila asione kama amenikosea mimi tu, aliwakwaza wengi,”


"Mimi na familia na watu wanaonizunguka, kuna watu wananiheshimu, wananifuatilia, wananiona kioo chao na wengine wananisapoti, hiki kilichotokea iwe fundisho hata kwa wengine pia kwani kwa kazi yake hivi vyombo ukivitumia vizuri vitakuongoza vema na kinyume chake utaangukia kubaya," amesema Mgunda
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad