Paula amuonya baba yake "Anamtukana mama yangu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Paula amuonya baba yake "Anamtukana mama yangu"


Uhusiano wa mtoto wa mwigizai wa Bongo Movies, Frida Kajala aitwaye Paula Kajala na babake mzazi P Funk Majani umeonekana kusambaratika zaidi baada ya Paula kumpa onyo babake mzazi.


Akizungumza katika kipindi cha ‘Behind The Gram’, Paula mwenye umri wa miaka 20 alisema kuwa hamheshimu babake mzazi kwa sababu kila mara yeye humsema vibaya mamake.


Paula vilevile anasema kuwa kitendo cha babake kumkataa hakikumkwaza hata kidogo.


"Mi nakutaga mtu sijui anajiita Paula Kajala sijui 'ohh I miss you daddy' si mtoto wangu sasa," Majani alisema katika mahojiano ya awali.


Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini Tanzania, Majani alilalamika kuwa Kajala alikuwa akimtangaza binti yake kwa dunia jambo ambao hakupendezwa nalo.


“Wanamuaibisha huyo binti. Kusema ukweli Kajala jinsi anavyomwanika hio ni tatizo na nishamwambiaga sana mamake ila mamake unajua halichukuli vile ye anachukulia kama sifa anajivunia binti yake," Majani alilalamika.


Inadaiwa kuwa P Funk Majani alimkana Paula, ambapo binti huyo aliacha kutumia jina lake na kuanza kujiita Paula Kajala.


“Namzungumzia baba. Mimi sihisi chochote kwa sababu yeye mwenyewe anakaana anamtukana mama huko kwenye vyombo vya habari," Paula alisema.


Paula pia amemwonya babake kukoma kuingilia maisha yake akisema kuwa kwa sasa yeye ni mwanamke aliyekomaa na hawezi kudhibitiwa kama mtoto mdogo.


"Sasa unafaa uniache niishi maisha yangu kama mwanamke sasa," Paula alimwambia Majani.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad