Ronaldo Anaswa Akiwa Amepaka Rangi ya Kucha Vidoleni, Sababu Zatajwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Jumatatu ya tarehe 26 mwezi Juni mwaka huu, Cristiano Ronaldo aliweka baadhi ya picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa mapumzikoni huku vidole vya miguu vya mwanasoka huyo vikiwa vimepakwa rangi nyeusi na kupelekea kuzua mjadala mkubwa.

Post hiyo ya Instagram iliyokuwa na maneno yaliyosomeka, “Vacation Mood” ilizua maswali kutoka kwa baadhi ya mashabiki wakimuuliza kwanini mwanasoka huyo alipaka rangi kucha zake.

Inavyoonekana, kupaka rangi kucha za miguu kwa wanasoka la kulipwa huchangiwa na sababu za kiafya, kama kusaidia kuzuia maambukizi na magonjwa mengine mabaya yanayohusiana na miguu.

Wanamichezo wengi mashuhuri hufanya hivyo ili kulinda kucha zao dhidi ya kuvu (Fungus) na bakteria kutokana na kuvaa viatu na kutokwa jasho kwa muda mrefu. Hata Mike Tyson aliwai kufanya hivyo, likiripoti jarida la Bild kutoka nchini Ujerumani.

Ronaldo hutambulika kwa kufanya kila jambo lenye matokeo chanya ili kumsaidia kuongeza urefu na ufanisi katika maisha yake ya kisoka.

Mshindi huyo wa Ballon d’Or mara tano, mara kwa mara hutumia bafu za barafu ili kurejesha haraka mwili wake kwenye hali ya utimamu, lakini pia ni muumini thabiti wa lishe bora.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 baada ya kuachana na Manchester United na kutimkia nchini Saudi Arabia mwezi Januari, ametumia muda huu wa mapumziko akiwa na familia yake pamoja na mchezaji mwenzake kutoka Timu ya Taifa ya Ureno Diogo Dalot, wakiwai kuitumikia kwa pamoja klabu ya Manchester United.

Na @Kubebekajr
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad