Atimae ALI Kiba Aingia Kibla, Marioo Amwimbisha Amapiano Baada ya Kuikataa Kwa Muda Mrefu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Atimae ALI Kiba Aingia Kibla, Marioo Amwimbisha Amapiano Baada ya Kuikataa Kwa Muda Mrefu


Sina haja ya kuongelea ukubwa wa Alikiba sababu sote tunaoipenda fleva ya Bongo tumempitisha kitambo tu, sina haja ya kuongelea ukali na ukubwa wa Marioo kwa sasa kwa sababu ndio Mkali ambaye usipopishana nae kwenye internet basi utapishana na migoma yake viwanjani na mitaani alafu kingine ni kwamba ana nyota zake 5 hata kwenye biti za amapiano.


Ninachotaka kukizungumzia hapa ni dude jipya linaitwa ‘sumu’ la Alikiba ft. Marioo ambalo limeachiwa usiku wa kuamkia leo na baada ya kulitambulisha rasmi @marioo_tz na @officialalikiba wakasimama mbele ya Taifa.


Kwanza wengi walikua wanataka kusikia Mwamba Kiba ataongea nini sababu iliwahi kuripotiwa kwamba hana mizuka na biti za amapiano…… alichosema ni hiki;


“Ni chemistry iliyonyooka, kila kitu Kina wakati wake na Marioo ni mdogo wangu, alikuja Nyumbani alitamani tufanye wimbo na hatimaye ndio huu, sio kwamba si-support muziki wa amapiano, muziki ni muziki.


“Sijachukia amapiano nilijiwekea tu, niliweza kufanya amapiano lakini nilimpa Abdukiba autumie ‘Hainogi’ ule wimbo ulitakiwa kuwa kwenye Album yangu lakini nilimpa Abdukiba akaufanya, amapiano ni muziki rahisi sana kufanya.


“Alikiba anapenda muziki mzuri, kazaliwa anafanya muziki mzuri, nilimuuliza kuwa nasikia amapiano haufanyi akasema mimi Sound yoyote nafanya ilimradi muziki mzuri,” amesema Marioo.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad